Saturday, March 28, 2009

Mkenya Mzalendo

Naishi, natumaini
Najitolea daima Kenya, Hakika ya bendera
Ni udhabiti wangu, Nyeusi ya wananchi na
Nyekundu ni ya damu
Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani
daima mimi mkenya, mwananchi mzalendo

Maneno haya si utenzi wangu mimi. Ni mwimbaji Eric Wainaina.

Nimekinai wimbo mwenyewe; kwani hadi sasa, hamna msanii mwingine ambaye ametupa kazi au wimbo ambao ni wa kizalendo na tena wenye kufikia kiwango cha kimataifa. Wimbo ambao ni wa kuburudisha na vilevile wenye ujumbe dhabiti - unaozungumzia wajibu wetu kama wananchi.

Mara ya kwanza kuusikia wimbo mwenyewe si juzi, la. Niliusikia miaka rudi - nikiwa shule ya upili papa hapa jijini nairobi. Kama wanakwaya shuleni, tulialikwa sherehe ya kutamatisha kibarua cha kukusanya mihela ambayou ingewaendea watoto waathiriwa kupunguza njaa humu nchini. Tulishinda njaa mchana kutwa na hela kiwango cha chakula cha mchana tukazikusanya. Tuliwapa wahisani tukitumaini na pia kuwaamini wazifikishe tulikokusudia.

Jioni baada ya haya yote, kijana mmoja ambaye wakati huo alikuwa akianzilia ulimwengu wa sanaa na uimbaji alikwea jukwaa. Kimya kilitanda mithili ya gubi gubi ya blankenti nzito alipoanza kuutirisha wimbo huu. Aliuimba kwa lugha ya kimombo na kwa kweli ungalilinganisha muziki wenyewe na mwingine wetu wakati huo, haungeamini ni utunzi na uimbaji wa mzaliwa.

Nisipoteze mada; wakenya lazima tuanze kujivunie ukwasi wetu wa lugha, wa utamaduni, wa manthari ya nchi, wa utaratibu wetu. Tusimame tisti, na kujivunia hali ii hii tuliyonayo. Tujivunie Kenya na Ukenya.

Video yenyewe: http://www.youtube.com/watch?v=TTzgA4t2Da0&feature=related

2 comments:

  1. Fahari wawili wapiganapo, ziumiazo ni Nyasi.

    Kama wakenya wazalendo, tungetafakari Maneno mazito yaliyomo kwenye wimbo huu. Bila shaka Kenya Ingekua Yakutamanika zaidi kweli.

    Changa moto....
    Wanasiasa wanaotaka kuona mbali bila kuzuiwa na miti ,wangechagua sehemu kama vile Marsabit ,Madera, Wajia, Isiolo kwa kutaja tu chache. Mbona wawachochee watu kwenda kuharibu Bustani zinazo tuwezesha kupata maji?. Hawafahamu maji ni uhai?

    Wakenya Tuungane, tuitunze Nchi yetu kwa kuiendeleza kuwa ya Kijani Kibichi.

    Nyekundu tuiache iwe tu kielelezo cha ukubusho wa umwagaji wa Damu.

    Tujivunia weusi tuliopewa na Maulana. Kwani hatufai kutenganishwa kiukabila.

    NCHI YETU YA KENYA,
    NI NCHI YA AJABUUU,
    TUUNGANE SOTE TUJENGE TAIFAA.
    ........
    .......
    KENYA NI NCHI YETU,
    TUNAIPENDA SAANA.

    WAKENYA WOTE TUUNGANE,
    TUJENGE NCHI PAMOJA.

    ReplyDelete
  2. Ilinibidi nitizame dakika kadha za kimya kutafakari na kuelewa uzito wa uliyoyaeleza kinagaubaga katika oni lako.

    Haswa usemapo damu iliyomwaika na iwe ni kumbukumbu tu, sio tukio la kila siku. Ni elimu ya aina hii itakayotusaidia kufahamu jukumu letu la kutunza uhai na kuangalia utukufu wa maisha.

    Ninakumbuka wimbo wetu we taifa:

    NATUJENGE TAIFA LETU
    EE NDIO WAJIBU WETU
    KENYA ISTAHILI HESHIMA
    TUUNGANE MIKONO
    PAMOJA KAZINI
    KILA SIKU TUWE NA SHUKRANI.

    James, asante kwa muda na maoni yako.

    ReplyDelete